Tuesday, August 14, 2012

ROBIN VAN PERSIE KUTUA MANCHESTER UNITED


ROBIN VAN PERSIE


ARSENE WENGER NA SIR ALEX FERGUSON
Kocha mkuu wa manchester united sir alex ferguson amekuwa na mazungumzo binafsi na kocha wa arsenal arsene wenger kuhusu uwezekano wa manchester united kukamilisha uhamisho wa mchezaji Robin Van persie.

Taarifa kutoka Mtandao wa Daily mail wa nchini uingereza unasema kwamba arsenal wanategemea kupata ofa nzuri kutoka kwa united kufuatia kuwepo kwa mazungumzo mazuri kati ya makocha wa timu zote mbili yaliyofanyika siku za karibuni.

Taarifa kutoka Vyanzo mbalimbali vya habari vinasema mpango wa kumhamisha mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga magoli 30 kutoka katika klabu ya arsenal ni lazima ukamilike wiki hii kabla ya kufunguliwa kwa pazia la ligi hiyo ambayo inaanza kupigwa rasmi mwishoni mwa wiki hii.

Inafahamika kwamba Meneja wa arsenal bwana wenger anahitaji kiasi cha paundi milioni 30 kutoka kwa manchester united ili iweze kumwachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 sasa lakini ipo tayari kusikiliza ofa inayoanzia paundi milioni 20 ambayo itakuwa na nyongeza ndani yake

Kikwazo pekee kinachomkumba alex ferguson ni namna ya kukamilisha mpango wa kumtwaa mchezaji huyo wa uholanzi kuja kucheza katika uwanja wa old trafford kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho arsenal wanahitaji ili waweze kumwachia mchezaji huyo na manchester united haiko tayari kutoa kiasi kikubwa cha fedha mabacho kinatakiwa na arsenal kwa mchezaji huyo.

Awali united walikaririwa kupewa ofa ya paundi milioni 30 kwa ajili ya mchezaji huyo na miamba hiyo miwili ya ligi kuu ya uingereza ilikubaliana kuhusu uhamisho huo lakini arsenal bado wanashikilia msimamo wao wa kuhitaji paundi milioni 30 na si chini ya kiwango hicho,

Uhamisho wa kushtua wa Van persie kutua Manchester united unaonekana kuwa suluhisho la kweli kwa mchezaji huyo ambaye awali iliripotiwa kuwa anahitajika na klabu za juventus ya italia na Manchester city ya uingereza

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed