
ASHLEY COLE
Mlinzi wa timu ya taifa ya England na timu ya chelsea Ashley Cole anatarajiwa kuiongoza timu ya taifa ya England kama kapteni wa timu ya taifa katika pambano la kirafiki dhidi ya jamhuri ya Ireland pambano litakalopigwa leo katika uwanja wa wmbley.Ashley cole ambaye ni beki kisiki wa timu ya chelsea na Timu ya taifa ya England atakuwa akiichezea england katika pambano lake la 100, na kocha wa timu ya taifa Roy Hodgson ameona ni fahari kwa mchezaji huyo kupewa ukapteni katika timu ya taifa kwa mchango wake mkubwa aliouonyesha kwa timu hiyo.
Kocha wa England Roy Hodgson akiongea na waandishi wa habari amesema kuwa cole ataongoza kikosi kama kapteni wa timu, lakini Frank lampard ataongoza kikosi endapo Steven Gerald hatakuwepo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed