Saturday, May 18, 2013

GERALD PIQUE NA ALEX SONG WAZICHAPA KAVU KAVU


 Gerard Pique (Kulia) na  Alex Song wakipigana mbele ya basi la Barcelona
Victor Valdes (kushoto) na Alexis Sanchez wakiangali wawili hao wakipigana
song akimpiga kibao pique
Wachezaji wa Barcelona Gerald pique na Alex song wameingia katika ugomvi baada ya wawili hao kuonekana wakizichapa kavi kavu mbele ya wachezaji wenzao wakati timu hiyo ikijiandaa kwa sherehe ya ubingwa wa hispania baada ya kufanikiwa kunyakua kikombe cha la liga kwa msimu wa 2012/2013. 

Alex song alionekana akimkunja Gerald Pique na alionekana akinyanyua mkono wake juu tayari kurusha ngumi kwa mchezaji mwenzake wa timu ya Barcelona. 

Wachezaji wote wa Barcelona walikuwa wakishuhudia tukio hilo wakati wakisubiri kupanda katika basi maalumu tayari kwa kuzunguka jiji la cataluna ikiwa ni moja ya sherehe za kufanikiwa kutwaa ubingwa wa La liga  kutoka kwa mahasimu wao Real madrid.

Chanzo cha ugomvi kati ya Gerald pigue na Alex song bado hakijafahamika

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed