KOLO TOURE
Timu ya soka ya Liverpool imefikia makubaliano na klabu ya Manchester city ya kumnyakua mlinzi wake mahili kutoka ivory coast Kolo Toure
Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ivory coast ambaye ana umri wa miaka 32 sasa atamaliza mkataba wake na klabu ya Manchester city ifikapo julai 1 mwaka huu na hivyo atakuwa tayari kutua katika klabu hiyo.
Toure amecheza michezo 102 akiwa na klabu ya manchester city tangu alipojiunga nayo akitokea arsenal kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 14 mwezi julai, 2009 na alikuwa mhimili wa klabu ya manchester city na kufanikiwa kunyakuwa kikombe cha ligi ya uingereza akiwa na klabu hiyo katika msimu wa ligi wa 2011-2012
Toure ambaye msimu wa ligi wa 2012-2013 haukumwendea vizuri alifanikiwa kucheza michezo 13 na aliachwa katika kikosi cha Timu hiyo ambacho kilishiriki katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.
Kolo Toure anajiunga na klabu ya Liverpool kufuatia kustaafu kwa mlinzi mwingine wa kati Jamie Carragher uku kukiwa na uvumi kwamba mlinzi mwingine wa kati kutoka slovakia Martin Skirtel ataiacha klabu hiyo mapema mwezi ujao.

No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed