Mwanzo mpya: Carlos Tevez akiwasili katika uwanja wa ndege wa Malpensa katika jiji la milan tayari kukamilisha mipango yake ya kuhamia Juventus
Carlos Tevez akiwa amezungukwa na Mashabiki wakiwa na hamu ya kumwona


Carlos Tevez akisalimia mashabiki wake

Carlos Tevez (Kushoto)
Mchezaji wa Manchester city Carlos Tevez yupo katika jiji la milan nchini Italia tayari kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya Juventus kwa ada ua uhamisho inayosadikiwa kuwa Paundi milioni 10.
Mchezaji huyo aliwasili katika uwanja wa ngehge wa Malpensa na kushuhudia umati mkubwa wa Mashabiki wakiwa wanamsubiri kwa hamu waweze kumwona.
Tevez mwenye miaka 29 sasa anatarajia kusaini mkataba wa miaka 3 na klabu ya Juventus baada ya kukamilisha uchunguzi wa afya yake leo ingawa taarifa za ndani zinathibisha kwamba mchezaji huyo bado hajakubaliana maslahi binafsi na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed