Sunday, June 02, 2013

CESC FABREGAS KUFANYA MAZUNGUMZO NA KOCHA TITO VILANOVA KUHUSU MUSTAKABALI WAKE BARCELONA

CESC FABREGAS AKISHANGILIA MOJA YA MABAO ALIYOIFUNGIA BARCELONA

Kiungo wa klabu ya Barcelona Cesc Fabregas anatarajiwa kukutana na kocha mkuu wa klabu ya Barcelona Tito Vilanova kujadili kuhusu mustakabali wake wa baadaye akiwa na timu hiyo huku kukiwa na tetesi kwamba Manchester united, manchester city na Arsenal zikiwa katika mawindo ya kumsajili kiungo huyo.
Mchezaji huyo angependa kubaki katika klabu hiyo ya Barcelona endapo atahakikishiwa kucheza akiwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha klabu ya Barcelona na hiyo inategemeana na majukumu ambayo klabu hiyo itampatia mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed