MARIO BALOTELLI AKIONDOKA KATIKA JIJI LA RIO DE JANEIRO BRAZIL, NYUMA YAKE NI MCHUMBA WAKE AITWAJE FANNY NEGUESHA
BALOTELLI ATAIKOSA SEHEMU ILIYOBAKI YA MASHINDANO HAYO
BALOTELLI AKIWA MBIONI KUONDOKA
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya italia na klabu ya AC Milan Mario Balotelli atakuwa nje ya mashindano ya kombe la mabara yanayoendelea nchini Brazil kutokana na kuumia nyama za paja katika pambano lililopita dhidi ya Brazil na hivyo kurejea nchini italia kwa matibabu zaidi.
Balotelli mwenye miaka 22 sasa atakosa mapambano yote yaliyosalia ikiwa ni pamoja na mechi ya nusu fainali dhidi ya hispania siku ya alhamisi na mapambano mengine yaliyobaki.
Mkuu wa kitengo cha matibabu cha Timu ya tiafa ya Italia amesema kupitia mtandao wa www.figc.it kuwa tatizo la balotelli ni kubwa na linahitaji matibabu ya haraka sana ili kuepusha matatizo makubwa yasije yakatokea kwa mchezaji huyo, hivyo nimewasiliana na kocha mkuu wa timu ya taifa Cesare Prandelli na kuamua kumrudisha Balotelli Katika jiji la milan kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed