Tuesday, July 09, 2013

BARCELONA YATUMA MAOMBI YA KUMNUNUA DAVID LUIZ KWA PAUNDI MILIONI 30

Barcelona wametuma maombi ya kumnyakua mlinzi wa klabu ya Chelsea David Luiz kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 30 lakini inaonekana chelsea hawapo tayari kumwachia mchezaji huyo kwa gharama hiyo.

Barcelona ambaye safu yake ya ulinzi inayumba yumba iko mbioni ipo mbioni kuongeza dau hilo ili iweze kumnyakua mchezaji huyo ili aweze kuwa mbadala wa Carles Puyol ambaye anakaribia kuachana na masuala ya soka ifikapo mwakani.

kumbukumbu zinaonyesha mchezaji huyo amekuwa mhimili mkubwa wa safu ya ulinzi tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea katika klabu ya soka ya Benfica januari mwaka 2011.

Mchezaji huyo ataweza kucheza sambamba na Gerald Pique na kufanya safu ya ulinzi ya klabu hiyo kuimarika zaidi, pia atweza kuungana na wachezaji wenzake wa brazil Dani Alves pamoja Neymar Da Silva Dosantos ambaye amejiunga na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed