
CRISTIANO RONALDO atastaafu Real Madrid hiyo ni kutokana na kauli ya Rais wa Real Madrid Florentino Perez.
Manchester united imejaribu kumrejesha mchezaji huyo wa ureno Old Traffold msimu huu lakini wiki iliyopita mchezaji huyo amethibitisha kwamba hayupo tayari kuikacha klabu hiyo yenye maskani yake Bernabeu na Rais wa klabu hiyo amesema Ronaldo anataka kustaafu soka hapa na sisi tungependa kuona mchezaji huyo akimaliza muda wake katika soka akiwa mchezaji wa Real madrid kama ilivyokuwa kwa Zinedine Zidane na wachezaji wengine wengi wenye majina makubwa.
Wakati huo huo Rais wa real madrid amethibitisha kwamba hajapokea maombi yoyote kutoka klabu ya Arsenal kuhusu uhamisho wa mchezaji Gonzalo Higuain ingawa amepata taarifa kutoka kwa baba mzazi wa Mchezaji huyo Jorge kwamba mchezaji huyo atajiunga na Arsenal kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 23
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed