
DAVID MOYES-KUSHOTO- AKIWA NA PHIL NEVILLE

RYAN GIGGS
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester united phil neville amerejea katika klabu ya manchester united kwa mara nyingine akiwa kama kocha wa kikosi cha kwanza cha united akisaidiana na Ryan giggs ambaye amepewa majukumu ya kuwa kocha mchezaji.
Neville ambaye ni mlinzi wa zamani wa klabu ya united alionekana akiingia katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya manchester united vilivyopo Carrington ambapo alitarajiwa kutangazwa kama kocha wa kikosi cha kwanza akisaidiana na makocha wengine walioteuliwa na David moyes katika harakati za kuendeleza gurudumu lililoachwa wazi na Sir Alex Ferguson, makocha wapya ni
Chris Woods, Steve Round, Robbie Cooke na Jimmy Lumsden ambao walikuwa wakisaidiana na moyes alipokuwa akiinoa klabu ya Everton.
Mkongwe Ryan Giggs (39) ambaye leseni yake ya UEFA inaisha mwezi ujao amepewa majukumu ya kuwa kocha mchezaji wa klabu hiyo baada ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed