
Everton wamemsajili dogo wa miaka 19 wa Barcelona Gerald Deolafeu kwa mkopo wa muda mrefu.
Deulofeu ambaye alikuwa anacheza timu "B" ya Barcelona ameweza kufunga mabao 18 katika michezo 33 aliyocheza.
Mchezaji huyo mwenye kipaji cha ajabu ameweza pia kucheza katika timu ya wakubwa ya barcelona pia alikuwa mhimili muhimu katika safu ya ushambuliaji katika timu ya taifa ya uhispania kwa vijana wa chini ya miaka 20 ambayo ilifanikiwa kunyakuwa ubingwa wa ulaya mwaka 2011/2012
Akiongea kuhusu mchezaji huyo kocha mpya wa everton Roberto Martinez amesema mchezaji huyo ni lulu kubwa katika soka la uhispania na pia ana kipaji kikubwa na cha ajabu sana.
Nimefurahi kwamba Gerald ameamua kuendeleza kipaji chake kwa kujiunga na Everton na ujio wake mahali hapa ni kitu muhimu sana kwake na kwetu pia alimalizia kusema Martinez
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed