
GERALD DEULOFEU
EBU ANGALIA MAAJABU YAKE HAPA
Everton na Tottenham wako mbioni kumsajili mchezaji mdogo mwenye maajabu anayecheza nafasi ya winga kutoka klabu ya Barcelona ya uhispania Gerald deulofeu.
Mchezaji hyo mwenye umri wa miaka 19 sasa amezivutia pia klabu za Arsenal na liverpool zote za uingereza ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa timu ya taifa ya umri chini ya miaka 20 kutoka nchini uhispania.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Barcelona lakini anaweza akapoteza nafasi kutokana na kuwasili kwa mchezaji machachari kutoka Brazil Neymar Da silva Dosantos.
Barcelona ilimsainisha mchezaji huyo mkataba wa miaka minne mwanzoni mwa mwaka huu lakini inafikiria kumtoa kwa mkopo kwa timu ambayo itafanikiwa kumnyakua katika kipindi hiki cha usajili.
Mchezaji huyo kwa sasa yupo katika mashindano ya kombe la dunia la vijana chini ya miaka 20 ambayo yanafanyika nchini uturuki na aliweza kufunga mara mbili katika ushindi wa uhispania wa mabao 4-1 dhidi ya Marekani.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed