Monday, July 01, 2013

MANUEL PELLEGRINI ATUA RASMI MANCHESTER CITY


KOCHA MPYA WA KLABU YA MANCHESTER CITY MANUEL PELLEGRINI AKIWA NA JEZI YAKE YA KLABU MPYA YA MAN CITY
Kocha mpya wa klabu ya manchester city Manuel pellegrini ametua rasmi katika klabu hiyo tayari kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na kocha wa zamani Roberto Mancini.

Kocha huyo kutoka nchini chile ameonekana akifanya ununuzi wa vifaa katika jiji la Manchester kabla ya utambulisho wake kama kocha mpya wa klabu ya man city.

Kocha huyo ameambatana na jopo la makocha ambao watakuwa wakifanya kazi pamoja nae, makocha hao ni 
Cousillas na kocha wa viungo Jose Cabello

Pellegrini (59) amejiunga na manchester city akitokea katika klabu ya Malaga ya hispania na anatakiwa kuleta mafanikio ya haraka katika klabu hiyo ili aweze kuwafanya wakuu na mashabiki wa klabu hiyo wawe na furaha.


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed