
MARKO VAN GINKEL
Timu ya chelsea ina amini kwamba mchezaji wake mpya Marko Van Ginkel atakuwa mrithi wa Frank Lampard katika klabu hiyo baada ya kukamilisha uhamisho wake wa paundi milioni 9 kutoka katika klabu ya Vitesse Arnhem.
Timu hiyo ya Darajani ilishinda vita vya kumsajili mchezaji huyo kutoka uholanzi ambaye alikuwa anawaniwa pia na klabu ya Ajax ya Amsterdam.
Chelsea imekuwa ikimwinda mchezaji huyo ambaye ametokea kuwa nyota wa uholanzi katika mashindano ya ulaya kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 21.
VAn Ginkel , 20, amekuwa akifuatiliwa na chelsea kwa miezi minne sasa wakiwa na mipango ya muda mrefu na mchezaji huyo atakapokamilisha uchunguzi wa afya yake wiki ijayo.
Mchezaji anaonekana kuwa mrithi sahihi wa Frank Lampard ambaye mwakani atatimiza miaka 35 na hivyo kuwa na wasiwasi wa kuweza kuachana na soka.
Van Ginkel alifanikiwa kufunga mabao 8 katika michezo 33 aliyoichezea klabu ya Vitesse msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed