
NICOLAS ANELKA
Klabu ya west brom imethibitisha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa Nicolas Anelka.
Anelka (34) ambaye ni mchezaji huru amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya west brom yenye makao yake Hawthorns.
Ikithibitisha usajili wa Anelka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter West Brom imesema:Klabu ya West brom imekamilisha usajili wa mchezaji Nicolas Anelka kwa mkataba wa mwaka mmoja uku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba wakiridhika na maendeleo yake, Kocha mkuu wa west brom Steve Clarke ambaye amewahi kufanya kazi na anelka katika klabu ya Chelsea amefurahishwa na usajili huo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed