Thursday, July 11, 2013

VICTOR WANYAMA AJIUNGA NA SOUTHAMPTON NA KUWEKA REKODI YA KUWA MKENYA WA KWANZA KUJIUNGA NA LIGI KUU YA NCHINI UINGEREZA

Mauricio Pochettino kushotoakiwa na Victor Wanyama 
Victor Wanyama aka Mugabe
Timu ya soka ya Southampton hatimaye imefanikiwa kumnyakua mchezaji wa nafasi ya kiungo Victor Wanyama kutoka katika klabu ya Celtic ya Scottland na kuweka rekodi ya uhamisho ya paundi milioni 12.

Victor wanyama (22) amesaini mkataba wa miaka 4 wa kuitumikia klabu ya southampton na kuikacha ofa iliyotolewa awali ya kujiunga na klabu ya Cardiff.

Mchezaji huyo mwenye uraia wa kenya akiongea kupitia mtandao wa kijamii wa twitter amesema anajisikia furaha kujiunga na Ligi kuu ya uingereza na kuwa mkenya wa kwanza kuichezea ligi hiyo yenye ushindani mkubwa lakini anajisikia huzuni kuiacha klabu yake ya Celtic.

Uhamisho wa mchezaji huyo umeufunika uhamisho wa paundi milioni 9.5 walizotoa Spartak Moscow kumnunua mchezaji Aiden McGeady kutoka klabu ya Celtic miaka mitatu iliyopita pia imeweza kuvunja rekodi kubwa ya uhamisho ya paundi milioni 12 ya klabu ya Rangers walipomuuza mchezaji Tore Andre Flo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed