
KOCHA WA MANCHESTER CITY MANUEL PELLEGRINI AKIWA NA TUZO YA KOCHA BORA WA MWEZI JANUARI
Kocha wa klabu ya Manchester City Manuel pellegrini ametajwa kama kocha bora wa mwezi februari baada ya kuiwezesha manchester city kumaliza mwezi januari wakiwa na rekodi bora katika ligi ya uingereza maarufu kama English Premier League, kwa kuiwezesha klabu hiyo kushinda mechi nne mfulilizo.
Ni tuzo ya pili mfululizo kwa kocha huyo baada ya kufanikiwa kuinyakua tuzo hiyo mwezi wa decemba .Tuzo hiyo imeshawahi kunyakuliwa mara mbili mfulilizo mwaka 2011na aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu ya chelsea Carlo Anceloti ambaye sasa anaifundisha klabu ya Real Madrid ya Uhispania.

MCHEZAJI BORA KWA MWEZI JANUARI ADAM JOHNSON AKIWA NA TUZO YAKE
Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi januari imekwenda kwa mchezaji wa Sunderland Adam Jonson baada ya kuweza kufanya vizuri katika mwezi huo kwa kufunga mabao 5.
Adam Johnson alionyesha kiwango cha ajabu kwa mwezi huo alipoweza kuisaidia klabu ya Sunderland(Black Cats) kutoka chini kwa kufunga bao 3(Hat trick) katika ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Fulham, pia aliweza kuisaidia klabu hiyo kiibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya New castle wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed