

PICHA MBILI JUU NI GARI AINA YA PORSCHE CAYENNE GTS YA LEWANDOWSKI INAVYOONEKANA BAADA YA KUIBWA TAIRI ZOTE NNE

ROBERT LEWANDOWSKI WA BORUSSIA DORTMUND
Mchezaji wa klabu ya Borussia Dortmund Robert Lewandowski amekuwa kwenye wakati mgumu sana na mashabiki wa klabu yake baada ya kutangaza kwake kujiunga na klabu ya bayern munich zote za ujerumani ambayo ni mahasimu wakubwa wa klabu ya Dortmund.
Kwa kuonyesha hasira mashabiki hao waliamua kutumia njia isiyo rasmi ya kumzuia mchezaji huyo kuondoka katika jiji hilo baada ya kuiba tairi katika gari lake la kifahari aina ya Porsche.
Mchezaji huyo aliamka siku ya ju8matatu asubuhi na kukuta gari lake likiwa halina matairi yote manne yakiwa juu ya mawe.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed