Saturday, February 22, 2014

WAYNE ROONEY ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED NA KUVUNJA UVUMI WA KUONDOKA OLD TRAFFORD

DILI IMEKAMILIKA
KUTOKA KUSHOTO NI MWENYEKITI MSAIDIZI WA MAN UNITED ED WOODWARD,WAYNE ROONEY NA KOCHA DAVID MOYES
WAYNE ROONEY KATIKATI AKISAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MITANO NA UNITED KULIA NI KOCHA WA MANCHESTER UNITED DAVID MOYES
WAYNE ROONEY AKIWA NA FURAHA BAADA YA KUSAINI MKATABA MPYA NA MANCHESTER UNITED

Mchezaji wa Manchester united Wayne Rooney siku ya Ijumaa alimshukuru kocha wa klabu ya Manchester united David kwa kuokoa maisha yake ya soka katika klabu hiyo baada ya kufanikiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomfanya kulipwa mshahara mnono wa paundi 300,000 kwa wiki.

Rooney aliiambia united kwamba alikaribia kuondoka klabuni hapo msimu uliopita baada ya kutokea kutoelewana kati yake na kocha wa zamani wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson na mabingwa hao wa england kupigana kumbakiza mchezaji huyo ambaye alikaribia kutua Chelsea kwa ada ya uhamisho iliyokadiriwa kufikia paundi milioni 30.

Moyes alithibitha kutaka kuondoka kwa mchezaji huyo kabla ya kufanya naye kikao cha siri ambacho kilimfanya mchezaji huyo kubaki klabuni hapo na kuhaidi kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika klabu hiyo. Mchezaji huyo amelipa fadhila kwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano utakaomfanya kuitumikia klabu hiyo mpaka mwezi june, 2009 na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi ya uingereza maarufu kama English Premier League.

Kulikuwa na uvumi mkubwa wa mimi kuondoka klabuni hapa katika majira ya joto lakini ujio wa kocha David Moyes ulibadilisha kila kitu kwa upande wangu.Nimekuwa na uhusiano mzuri na kocha David Moyes tangu nilipokuwa kijana mdogo katika klabu ya Everton, ameweza kuniamini na kuonyesha matumaini makubwa sana kwangu.

Nafurahi kuwa katika klabu kubwa duniani na kuweza kuitumikia kwa moyo wangu wote na kumalizia maisha yangu ya soka nikiwa mahali hapa ni kitu muhimu sana kwangu.

Nafurahi kwa kuwa hatimaye mambo yote yameisha na kunifanya niweze kuweka nguvu zangu zote katika mafanikio ya timu yangu, nilikuja manchester united nikiwa na miaka 18 na sasa nakaribia miaka 30 na hiyo itafanya maisha yangu yote ya soka yamalizie mahali hapa.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed