Timu ya soka ya Manchester united ambayo msimu huu imekuwa ikienda kwa mwendo wa kinyonga katika ligi kuu ya nchini uingereza hapo jana ilizinduka kutoka katika lindi la usingizi kwa kufanikwa kuichapa klabu ya West brom kwa mabao 3-0 na kuondoa ukame wa kutoshinda mechi nyingi za ugenini msimu huu.
Pambano lilianza kwa kasi uku kila timu ikiwa na shauku ya kuliona lango la mwenzakelakini kila moja ilishindwa kuliona lango la mwenzake.
Iliwachukua united dakika 34 kuweza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Phil Jones kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Robin Van Persie.
Dakika ya 65 wayne Rooney aliweza kuiandikia united bao la pili kabla ya Danny welbeck aliyeingia katika dakika ya 63 kuchukua nafasi ya Robin Van Persie kufunga bao la tatu katika dakika ya 82 na kufanya pambano hilo kumalizika kwa united kutoka kifua mbele kwa bao 3-0.
Katika pambano hilo mchezaji Rafael Da Silva wa manchester united alitajwa kama mchezaji bora wa pambano hilo



WAYNE ROONEY AKIIFUNGIA UNITED BAO LA PILI KWA KICHWA


PHIL JONES AKIFUNGA
BAO LA KWANZA KWA KICHWA

DANNY WELBECK AKIIFUNGIA UNITED BAO LA TATU
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed