WACHEZAJI WA BAYERN WAKISHANGILIA MOJA YA USHINDI WAO KATIKA MASHINDANO YA KOMBE LA MABINGWA
UWEZEKANO WA ARSENAL KUSHINDA PAMABNO LA LEO UKIWA KATIKA ASILIMIA
WACHEZAJI WA ARSENAL WAKIWA MAZOEZINI KUJIANDAA NA PAMBANO LA LEO USIKU DHIDI YA BAYERN MUNICH
Timu ya soka ya Arsenal inatupa karata yake ya mwisho leo katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya katika pambano ambalo linasadikiwa kuwa gumu kuliko yote(Mission Impossible) pale watakapokipiga na timu ya Bayern Munich ya ujerumani katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya pambano litakalopigwa leo katika uwanja wa Allianz uliopo katika jiji la Bayern nchini ujerumani.
Arsenal wanashuka katika pambano hilo wakikumbuka kipigo cha bao 2-0 walichokipata wiki iliyopita katika uwanja wa Emirates na hivyo inawalazimu kufanya jitihada kubwa kuweza kushinda kwa ushindi usiopungua goli tatu na kuendelea.
Timu ya soka Bayern ambayo inashuka dimbani ikiwa na kiwango bora kabisa kwa msimu huu inahitaji sare ya aina yoyote ile au ushindi wa aina yoyote ile iweze kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya mashindano hayo makubwa kabisa kwa upande wa klabu barani ulaya.
Kutokana na takwimu zilizotolewa na mtandao wa Opta klabu ya soka ya Bayern ambayo inashiriki katika ligi ya bundesliga ya nchini ujerumani katika michezo sita iliyopita ya ligi hiyo klabu hiyo iliweza kuwabana wapinzani wake na hivyo kuweza kudhibiti lango lake hata wasingekuwa na kipa katika lango lao.Mwache golikipa Manuel Nour akiwa katika benchi bado klabu hiyo ingeweza kucheza vizuri na kushinda mapambano yake wakiwa na moto ule ule.
Katika msimu wa 2013/2014 timu ya Bayern munich imeweza kufungwa magoli 3 tu kwa mwaka 2014 na moja ya magoli hayo ni goli la kujifunga katika ushindi wa magoli 5-1 walioupata dhidi ya klabu ya schalke 04 mwanzoni mwa mwezi machi.
Arsenal walipata kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Bayern katika uwanja wa Emirates katika pambano ambalo Mesut Ozil alikosa penati na hivyo kuwafanya Arsenal kuwa katika wakati mgumu katika pamabno la leo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed