Wednesday, September 05, 2012

ANGELO ENRIQUEZ AJIUNGA RASMI NA MANCHESTER UNITED


ANGELO ENRIQUE AKIWA NA JEZI YAKE MPYA YA MANCHESTER UNITED
ANGELO ENRIQUE AKISAINI MKATABA WA MANCHESTER UNITED PEMBENI YAKE NI SIR ALEX FERGUSON
AKIWA OLDTRAFFORD
Hatimaye Manchester united imethibitisha kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 18 Angelo Enriquez kutoka katika klabu ya universidad de chile ya nchini chile .

Mchezaji huyo kutoka chile amekamilisha vipimo vya afya na kutua rasmi katika klabu ya manchester united kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 4.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya universidad de chile alifanikiwa kufunga magoli 11 katika michezo 17 aliyoichezea klabu yake ya zamani katika msimu uliopita na kuweza kuisaidia timu yake kunyakua taji la ligi hiyo.

Akimwongelea mchezaji huyo kocha wa manchester united sir alex ferguson amesema mchezaji huyo ni hazina kubwa kutokana na kasi na uwezo wake mkubwa wa kuweza kuusoma mchezo awapo uwanjani, ni mchezaji wa aina yake kwa umri mdogo alionao
.
Tuna sifa ya kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi na angelo anafaa kuingia katika rekodi za manchester united kutokana na uwezo wake alionao.

Akiongea na mtandao wa manchester united mchezaji huyo amesema anajisikia furaha kuwa mahali hapo na kuendelea kusisitiza kwamba manchester united ni timu kubwa duniani na inaongozwa na kocha bora kabisa duniani.

Manchester united imethibitisha mchezaji huyo atakuwa anavaa jezi namba 21

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed