Friday, September 07, 2012

SIWEZI KUONDOKA BARCELONA ASEMA CESC FABREGAS

CESC FABREGAS AKIWA MAZOEZINI NA WACHEZAJI WENGINE WA BARCELONA
Mchezaji wa kiungo wa timu ya Barcelona Cesc Fabregas amesema hawezi kuondoka katika klabu ya Barcelona na anapenda kumalizia maisha yake ya soka akiwa katika klabu hiyo pamoja na kutanganza kwamba hana furaha na majukumu yake katika klabu hiyo.

Mchezaji huyo wa zamani ya Arsenal ya uingereza alijiunga na klabu yake aliyojifunzia kucheza soka katika msimu wa m,ajira ya joto uliopita kwa ada ya paundi milioni 35 lakini amekuwa chaguo la pili katika roho ya kiungo ya timu ya Barcelona nyuma viungo mahili wa Barcelona Xavi Hernandez na Andres iniesta

Fabregas alipata nafasi ya kuanza katika mechi ambayo Barcelona ilipata ushindi mdogo dhidi ya Valencia Jumapili iliyopita lakini aliishia kucheza kwa dakika 63 tu kitu kilichomfanya kusema kwamba hakupendezewa na kutolewa katika pambano hilo. Siku zote nawaombea vizuri wachezaji wenzangu na ninawaonyesha uso wa furaha lakini moyoni ninakuwa na majonzi na siwezi kuonyesha hali hii kwa wachezaji wenzangu.

Taarifa za kukuwa na furaha kwa Fabregas kumekuja baada ya mchezaji maarufu wa timu ya real madrid Cristiano Ronaldo kuripotiwa kutokuwa na furaha katika klabu yake ya real madrid kutokana na sababu za kimpira na si fedha kama mwenyewe alivyosema.

Akiongelea habari hizo Fabregas amesema hana nia ya kuikacha klabu hiyo na kuendelea kusisitiza kwamba mambo hayo yamekuzwa sana na vyombo vya habari, nina furaha na niko kwenye klabu na ninapenda kuwa hapa kwa miaka mingi zaidi

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed