Wednesday, October 30, 2013

YAYA TOURE ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA MAZINGIRA WA UNEP



YAYA TOURE AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKURUGENZI MKUU WA UNEP ACHIM STEINER KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI

YAYA TOURE AKIWA KATIKA SEHEMU MAALUMU YA KUTUNZIA TEMBO NCHINI IVORY COAST
YAYA TOURE AKIWA KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI JIJINI NAIROBI
YAYA TOURE AKITIA SAHIHI KATIKA KITABU CHA SHABIKI WAKE

Kiungo wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester city ya Uingereza Yaya Habib Toure ametajwa kama balozi wa uhamasishaji wa mazingira wa UNEP (United Nations Environmental Programme) kuhusu kupiga vita uwindaji haramu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Vory Coast ameingia katika kampeni hiyo yenye lengo la kupiga vita uuaji wa Tembo huku akisisitiza kuwa katika nchi ya Ivory Coast wamebaki Tembo wanaofikia 800 tu.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano maalumu uliofanyika katika jiji la Nairobi nchini Kenya Yaya Toure amesema uwindaji haramu ni hatari sana na unatishia kumaliza kabisa kizazi cha Tembo walipo katika bara la Afrika na kama hatutachukua hatua za haraka kuna hatari ya kupoteza kizazi chote cha Tembo katika miaka ijayo.

Timu ya Taifa ya Ivory Coast inatumia jina la utani la Tembo kutokana na jinsi viumbe hao wa ajabu walivyo na nguvu na maumbile ya kuvutia.

Mkurugenzi mkuu wa UNEP Achim Steiner akimkaribisha Yaya Toure amesema mchezaji huyo ni sauti kubwa katika bara la afrika ambaye ataongeza chachu ya kupambana na changamoto za mazingira. 


No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed