Sunday, November 03, 2013

ARSENAL YAINYAMAZISHA LIVERPOOL EMIRATES YAIFUMUA BAO 2-0 SUARES NA DANNY STURRIDGE WASHINDWA KUTAMBA UGENINI


Ligi ya soka ya nchini England iliendelea hapo jana kwa kuzikutanisha timu mbalimbali nchini humo.vinara wa ligi hiyo Liverpool walikuwa ugenini katika uwanja wa Emirates kupambana na Arsenal ambapo vinara hao walijikuta wakishindwa kutamba mbele ya vijana wa Arsene wenger kwa kuambulia kipigo cha mabao 2-0 uku washambuliaji wake machachari Luis Suares na Danny Sturridge (SAS) wakishindwa kufurukuta mbele ya safu ya ulinzi ya Arsenal iliyokuwa ikiongozwa na Per Mertesacker ambaye alisimama imara akisaidiana na walinzi mwenzake akina vamalen , koscielny na Bacary sagna ambao walisimama vizuri kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Liverpool.

 Mabao ya Arsenal yaliwekwa kambani na Saint Carzola aliyefunga katika dakika ya 19 baada ya kuidaka pasi ya pembeni ya bacary sagna na hivyo kuweza kufunga bao hilo baada ya mpira wa kichwa kugonga mwamba wa juu na bao la pili lilifunga wa Aaron Ramsey baada kuizidi ujanja ngome ya Liverpool iliyokuwa ikiongozwa na Kolo Toure aliyeonekana kufanya makosa mengi ya kizembe.
SAINT CARZOLA AKIIFUNGIA ARSENAL BAO LA KWANZA
RAMSEY AKIIFUNGIA ARSENAL BAO LA PILI

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed