Sunday, November 10, 2013

CRISTIANO RONALDO APIGA HAT TRICK REAL MADRID WAKIIPIGA REAL SOCIEDAD BAO 5-1


CRISTIANO RONALDO:LEVEL NYINGINE
CRISTIANO RONALDO AKISHANGILIA HAT TRICK ALIYOFUNGA KATIKA MECHI YA JANA DHIDI YA REAL SOCIEDAD
CRISTIANO RONALDO AKIPONGEZWA NA GARETH BALE BAADA YA KUFUNGA HAT TRICK
GARETH BALE KATIKA HARAKATI ZAKE UWANJANI
KARIM BENZEMA AKIPONGEZWA BAADA YA KUFUNGA BAO LA PILI
SAMI KHEDIRA AKIIFUNGIA REAL BAO LA NNE

VIKOSI

REAL MADRID: López, Carvajal, Arbeloa, Alonso (Illarramendi 70), Varane, Pepe, Khedira (Isco 77), Modric, Benzema (Morata 83), Bale, Ronaldo
WACHEZAJI WA AKIBA: Casillas, Nacho, Jesé, Di María
MAGOLI: Ronaldo 12, 26 (p), 76, Benzema 18, Khedira 36


REAL SOCIEDAD: Bravo, Martínez (Ansotegi 59), José Ángel, Elustondo (Zurutuza 45), González,  Iñigo Martínez, Vela, Bergara, Seferovic (De la Bella 45), Xabi Prieto, Griezmann
WACHEZAJI WA AKIBA: Aggiretxe, Zubikarai, Castro, Javi Ros
MAGOLI: Griezmann 61

Ikionekana kama ni kujibu shutuma na kejeli zilizoelekezwa kwake na Rais wa shirikisho la soka duniani (FIFA) Sepp Blater alipotoa maneno ya dhihaka dhidi yake kwamba si chochote katika uchezaji wa soka lake na kwamba kwake yeye Lionel Messi ni zaidi kwa kila kitu dhidi ya mreno huyo.

Cristiano Ronaldo akicheza katika pambano la jana dhidi ya Real sociedad ameweza kuionyesha dunia kwamba yeye ni zaidi pale alipoweza kufunga mabao matatu yaani hat trick na kuiwezesha klabu yake ya Real madrid kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1 uku wachezaji wengine Karim Benzema na Sami Khedira wakifunga moja kila mmoja na kuing'arisha klabu ya real madrid

Mashabiki waliofurika katika uwanja wa Santiago Bernabeu hapo jana walijikuta wakiimba wimbo wa Ronaldo Ballon d'Or' wakiamini kwamba mchezaji huyo ndiye anayestahili kunyakua tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia wa FIFA.

Tangu alipopigwa madongo na Rais huyo Cristiano Ronaldo amekuwa hashikiki baada ya kufanikiwa kufunga mabao 9 katika mechi 4 alizocheza na ameweza kuwa na mabao 62 mpaka sasa kwa mwaka huu na akiwa amefunga hat trick ya 19 tangu ajiunge na real madrid akitokea klabu ya manchester united ya uingereza.

Akiongelea kiwango chake mchezaji huyo amesema hawezi kuvunjwa moyo na maneno ya kejeli ya Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter yeye anachojali ni kucheza soka na kuwaachia watazamaji waamue kila kitu.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed