Tuesday, November 05, 2013

JOE HART KUENDELEA KUSUGUA BENCHI MAN CITY

JOE HART
Kipa nambari moja wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester city Joe Hart ataendelea kusugua benchi leo katika pambano la klabu bingwa barani ulaya wakati Manchester city itakaposhuka dimbani leo usiku katika uwanja wa Etihad kuwavaa CSKA Moscow hiyo ni kutokana na maelezo ya kocha wa klabu hiyo Manuel Pellegrini.

Joe hart alipigwa chini katika pambano la ushindi wa bao 7-0 walioupata manchester city dhidi ya Norwich city wikiendi iliyopita uku nafasi yake ikikamatwa na Costel Pantilimon mlinda mlango kutoka Romania

Akiongelea pambano la leo usiku kocha wa manchester city Manuel Pelegrini amesema Golikipa kutoka Romania Costel Pantilimon ataendelea kukaa golini leo wakati timu hiyo itakapowakaribisha CSKA kutoka Urusi.

Sifahamu ni lini Mlinda mlango huyo atarudi golini, tutaangalia baadaye nini cha kufanya alisema Pellegrini.

Joe hart (26) amekuwa na wakati mgumu katika klabu ya manchester city kufuatia makosa kadhaa aliyoyafanya katika mapambano yaliyopita ikiwa ni pamoja na uzembe katika pambano la tarehe 27 oktoba ambapo City walikosa pointi baada ya kujikuta wakichapwa bao 2-1 na chelsea.

Pellegrini amesisitiza kwamba ni muhimu kwa kipa huyo kupata mapumziko kwa muda kidogo baada ya kuitumikia klabu hiyo akiwa mlinda mlango namba moja kwa muda wa miaka miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed