Saturday, March 24, 2012

AU KUANZISHA OPERESHENI KALI YA KUMSAKA KIONGOZI WA LRA JOSEPH KONY

Joseph Kony, kiongozi wa kundi la kigaidi la LRA linalopigania kuunda serikali ya Kikristo chini ya amri 10 za Biblia nchini Uganda 
moja wa Afrika unatarajiwa leo kuanza operesheni kali ya wanajeshi 5,000 huko mjini Juba, Sudan Kusini, kwa lengo la kumsaka Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa LRA wanaopigania kuunda serikali ya Kikristo inayoongozwa kwa amri 10 za Biblia nchini Uganda. 
Operesheni hiyo ambayo itaongozwa na serikali ya Kampala chini ya usimamizi wa AU itawajumuisha pamoja askari wa Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati. 
Fransisco Madeira, Mwakilishi Maalum wa AU katika operesheni hiyo amesema kwamba, kikosi hicho kitapiga kambi katika mji wa Sudan Kusini wa Yambio karibu na mpaka wa Kongo DRC, na askari watapelekwa katika maeneo ya msituni ambako Kony na wafuasi wake ndiko wanakojificha. 
Wiki iliyopita Waziri wa Ulinzi wa Uganda alisema kuwa, kampeni hiyo inahitajia msaada zaidi wa kimataifa. 
Kony anasakwa kwa udi na uvumba na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kwa kosa la kutenda jinai za kivita, kuwateka nyara watoto wadogo na kuwatumia kama askari vitani, kuwateka nyara wanawake na kuwafanya watumwa wa ngono pamoja na jinai nyinginezo.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed