LONDON, ENGLAND
WAYNE Rooney, ambaye kikosi chake kitapambana na Tottenham kesho Jumapili, amesema ana uhakika kuwa watapata ubingwa wa Ligi Kuu England kwa sababu wachezaji wa Manchester United hawana kawaida ya kuchanganyikiwa.
SOURCE: MWANASPOTI
Manchester United imerudi katika kiwango katika siku za karibuni ambapo mwezi uliopita walitoka nyuma kwa mabao 3-0 na kutoka sare ya mabao 3-3 na Chelsea huko Stamford Bridge na wiki iliyopita waliifunga Norwich mabao 2-1. Rooney anasema anaamini wataendelea kufanya vizuri zaidi.
Lakini Rooney anaongeza kuwa hakuwa na imani hiyo wakati alipojiunga Manchester United mwaka 2004.
Wakati nilipohamia katika klabu hii nikiwa na umri mdogo nilikuwa napata mashaka wakati tunapofungwa. Lakini sasa nimekuwa mtu mzima, nina uzoefu wa kutosha, tunapofanya makosa, huwa hakuna sababu ya kuchanganyikiwa bali tunapata ari zaidi.
Kujiamini huku kunatokana na kucheza mechi nyingi na kupata uzoefu wa kutosha.
Lakini, Manchester United ilikuwa na wakati mgumu wiki iliyopita wakati ilipolazimika kusawazisha bao dakika ya 83 kwenye mechi dhidi ya Norwich na baadaye wakapata bao la ushindi dakika za lala salama kupitia kwa Ryan Giggs na kuendelea kuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi mbili.
Nyota huyo mwenye miaka 26 amesema mechi dhidi ya Chelsea ilitosha kuionyesha Manchester City kwamba wanaweza kufanya maajabu wakati wowote.
Kila mtu aliyeangalia mechi hiyo alifahamu kuwa huwa hatukati tamaa, huwa tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunapata pointi muhimu.
Wakati timu nyingine zinapokuwa nyuma kwa mabao 3-0 hukata tamaa na hujipanga kuzuia mabao mengine yasifungwe, alisema.
Rooney atakuwemo katika kikosi kesho Jumapili baada ya kukosekana katika mechi dhidi ya Norwich na mechi ya kirafiki kati ya England na Uholanzi.
Tunatakiwa kucheza kwa umaniki ili kupata ushindi, alisema.

No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed