Azam Academy yaitoa jasho Azam FC, Kurudiana Jumamosi Asubuhi

Japokuwa wamefungwa 2-1 lakini timu ya Azam Academy wamewapelekesha vilivyo kaka zao Azam FC kwenyemchezo wa kujipima nguvu uliopigwa jana asubuhi, kwenye uwanja wa Azam, Chamazi.
Timu hizo zinajiandaa na mashindano, Academy wanajiandaa na mashindano ya Rollingstone 2012 yatakayofanyikanchini Burundi wakati Azam FC wao wanajiandaa na mashindano ya Kombe la Kagame yatakayofanyika Dar esSalaam mwezi ujao.
Academy walicheza kandanda safi muda wote wa mchezo na kuwapa wakati mgumu Azam FC kutokana na uwezowa wachezaji hao.
Vijana hao walio chini ya miaka 20 ingawa wengi wao ni chini ya miaka 17 wamecheza mchezo huo siku mojabaada ya kuifunga timu ya Iringa United kutoka mkoani Iringa mabao 7-0.
Katika mchezo dhidi ya Azam FC ambao Academy walifungwa 2-1, Academy walikuwa wa kwanza kupata bao lamapema katika dakika ya tano ya mchezo kupitia kwa Joseph Kamwaga aliyeachia shuti lililomshinda kipaDeogratias Munishi ‘Dida’ wa Azam FC. Kimwaga ambaye anaaminika kuwa ndiye winga mwenye kasi zaidi nchinikwa sasa ambeye pia anachezea timu ya taifa ya Under 20 alikuwa mwiba kwa mabeki wa Azam FC muda wote wamchezo.
Goli hilo lilidumu hadi mapumziko huku timu hiyo ikiwanyanyasa kaka zao kwa kuwaonyesha uwezo wao imarauliojengeka kutokana na mazoezi bora wanayopata chini ya makocha wao Nagul Vivek na Iddi Cheche.
Azam FC walitafuta nafasi ya kushinda lakini timu hiyo iliyocheza kipindi cha kwanza ikiongozwa na GaudenceMwaikimba haikuweza kubadilisha matokeo hayo.
Kipindi cha pili kilianza vizuri vijana walikuja kwa kasi na kuzuia mashambulizi ya kaka zao Azam FC, lakini dakikambili za mwisho makosa ya benchi la ufundi la Academy ya kubadilisha timu yao ili kutoa nafasi kwa wachezaji zaidikupata nafasi ya kucheza yalipelekea Azam FC kutumia nafasi hiyo kusawazisha goli na kuongeza goli la Ushindi.
Goli la kwanza kwa Azam FC liliwekwa wavuni na mshambuliaji George ‘Blackberry’ Odhiambo kwa shuti la pembenina goli la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Zahoro Pazi kwa shuti la mbali nje ya eneo la penati.
Timu hizi zitarudiana siku ya Jumamosi Asubuhi ambapo kambi zote mbili zimetamba kushinda mchezo huo.
Kabla ya hapo hapo kesho asubuhi Azam Academy itashuka kwenye uwanja wa JKT Ruvu kukwaana na JKT Ruvu.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed