Monday, July 09, 2012

KUTOKA AZAM FC


Azam FC kukwaana na Super Falcon katika nusu fainali ya Urafiki Cup
Timu ya Azam FC leo itacheza mchezo wake wa nusu fainali ya mashindano ya Urafiki Tanzania dhidi ya mabingwawa Zanzibar, Super Falcon kwenye uwanja wa Amaan visiwani hapa.

Azam FC imejiandaa kikamilifu kucheza mchezo huo na kupata ushindi ili wapate nafasi ya kucheza fainali zamashindano hayo zitakazofanyika siku ya Jumatano.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala alisema wameajiandaa vizuri kucheza mcheza mchezo huo kwa kuwawachezaji wote wana hali nzuri.

Akizungumzia Super Falcon, Kali alisema timu hiyo ya kutoka Pemba haina tofauti na zingine kwa kuwa zinachezampira wa aina moja na wameshacheza na timu mbili hivyo hawatawapa shida.

“Sisi tupo vizuri, timu za huku zinafanana aina ya uchezaji huwa wanapigana hadi mwisho wa mchezo tumejiandaakwa hilo lakini lolote linaweza kutokea huu ni mpira” alisema Kali.

Aliogeza kuwa mazingira ya uwanja ni changamoto kwa wachezaji wake kwa kuwa uwanja huo hauna kiwango kizurikwa kuchezea

Azam Academy yaanza kwa kishindo Rolling Stone nchini Burundi

Azam Academy imeanza vizuri mashindano ya Rolling Stone baada ya kuisasambua timu ya Nyirakongo ya DRC 3-0,

Magoli yamefungwa na kimwaga (2) Mudathir (1) katika mchezo ambao Azam Academy waliutawala mchezo mudawote

Timu iliyoanza jana ni Aishi, Mgaya,Shabalala,Dizana,Mkomola, Reyna, Mudathiri,Kaijage,Machupa, Kelvin andKimwaga.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed