Friday, July 20, 2012

JOSE BOSINGWA APATA DILI YA KUKIPIGA ANZHI MAKHACHKALA

Mshindi mara mbili wa ubingwa wa england akiwa na timu ya chelsea Jose Bosingwa amepata ofa ya kukipiga katika klabu ya Anzhi Makhachkala. Mchezaji huyo ambaye ameachwa na timu ya chelsea baada ya kumaliza mkataba wake akiwa na timu hiyo amekuwa huru na yuko tayari kujiunga na timu yoyote itakayomhitaji.Mchezaji huyo ambaye amepata mafanikio akiwa na klabu ya chelsea pamoja na kufanikiwa kunyakua ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya ni mmoja wa mabeki wazuri wa pembeni ambaye timu yoyote ingehitaji kuwa naye.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed