BALE AKIWA KATIKA MAZOEZI BAADA YA KUPATA NAFUU
BALE AKIWA CHINI KWA MAUMIVU BAADA YA KUCHEZEWA RAFU MBAYA NA ADAMS
Kocha wa Tottenham hotspurs Andre villas boas amepata ahueni baada ya kusikia taarifa kutoka kwa madaktari kwamba winga wake machachari gareth balle yuko vizuri baada ya kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa liverpool charlie adams katika mechi ya kirafiki ambayo ilimshuhudia winga huyo akitolewa nje katika machela baada ya kufanyiwa rafu hiyo mbaya.
Kocha huyo wa ureno amemtaka mchezaji huyo kutoka scotland ambaye anakipiga katika klabu ya Liverpool kuomba samahani kwa rafu mbaya ambayo amemfanyia balle ambaye alitoka uwanjani akiwa amevalishwa kiatu maalumu cha kuulinda mguu wake.
Gareth balle alipata maumivu hayo wakati anichezea timu yake ya Tottenham katika mechi ya kirafiki uko Baltimore marekani ambapo timu hizo zilitoka sare ya 0-0 katika mechi ya kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya uingereza.
Taarifa za madaktari zimethibitisha kwamba mchezaji huyo hakupata majeraha katika mguu wake na hivyo anaruhusiwa kuendelea na mazoezi kwa ajili kujiweka sawa kwa msimu ujao wa ligi
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed