
Klabu ya soka ya Paris st German inakaribia kumnyakua mshambuliaji hatari wa AC Milan Zlatan Ibrahimovic, akiongea kwa nyakati tofauti mkurugenzi wa michezo wa Paris St. German Leonardo amesema timu hiyo iko mbioni katika harakati zake za kutengeneza kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ya ufaransa na hivyo ujio wa ibrahimovic utaongeza chachu ya ushindani katika ligi hiyo maarufu kama League 1.
Wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa sweden alitumia muda wa siku kadhaa katika mji mkuu wa ufaransa paris akijaribu kuweka sawa mambo ya uhamisho wa mchezaji huyo baada ya klabu ya Ac milan maarufu kama Rossoneri kukubali kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 pamoja na mchezaji mwingine Thiago silva katika klabu ya PSG.
Taarifa kutoka italia zinasema mchezaji huyo amekubali ofa ya Euro milioni 13 kwa mwaka pamoja na ada ya uhamisho ya Euro milioni 23 kutoka kwa PSG.
Akiongea na Gazeti la Gazeta Dello Sport mkurugenzi wa michezo wa PSG leonardo amesema tumefikia makubaliano na Zlatan ibrahimovic ni mchezaji wetu na anakaribia kuweka historia katika klabu hii.Wakala wa Ibrahimovic Mino Raiola akiongea na waandishi wa habari amethibitisha kufanyika kwa dili hilo na kwamba pande zote mbili zimefurahi kukamilisha uhamisho huo.
wakati huo huo klabu ya PSG imehitisha mkutano ambao utafanyika siku ya jumatano ambapo mkurugenzi wa michezo Leonardo pamoja na Rais wa klabu hiyo bwana Nasser Al Khelaifi watakuwepo kukiwa na lengo la kumtambulisha ibrahimovic pamoja na mchezaji mwingine mdogo aitwaye Marco Verratti aliyejiunga na klabu hiyo akitokea katika klabu ya pescara
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed