Kevin de Bruyne
Timu ya Chelsea imeamua kumtoa kinda wake Kevin de bruyne kwenda kupata uzoefu wa kiushindani katika soka katika klabu ya Werder Bremen ya ujerumani.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 raia wa ubelgiji aliwasili katika klabu ya chelsea katika dirisha dogo la usajili la januari akitokea katika klabu ya Genk kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 7 kabla ya kurudi tena kwenye klabu hiyo kwa mkopo.
Alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na chelsea katika mechi ya ushindi wa bao 4-2 ambao chelsea iliupata dhidi ya seattle sounders ya marekani katika ziara ya chelsea nchini marekani kuweza kujiweka fiti kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya nchini uingereza lakini chelsea imeona bado anahitaji kupata uzoefu zaidi na hivyo kuamua kumtoa werder bremen kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed