Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya England Manchester City watachuana na mshindi wa mara tisa wa mabingwa wa Ulaya Real Madrid katika hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya.
Timu ya Roberto Mancini itachuana pia na Ajax pamoja na Borussia Dortmund.
Mshindi wa hivi sasa wa Ligi hiyo Chelsea anaanza utetezi wa taji lake kwa mchuano dhidi ya Juventus, huku Celtic ikiwa imepangwa kuminyana na Barcelona katika kundi G.
Manchester United inapambana na Galatasaray, Braga na FC Cluj huku Arsenal ina Schalke, Olympiakos na Montpellier kwenye kundi lao la B.
Chelsea, iliyoibwaga Bayern Munich kupitia mikwaju ya peneti katika fainali iliyochezwa ndani ya uwanja wa Bayern msimu uliopita hivi sasa inakabiliana na upinzani wa Shaktar Donetsk kutoka Ukraine na FC Nordsjaelland ya Denmark na Juventus.
Pamoja na Barcelona, Celtic ina mlima wa kusafiri kwenda Benfica na pia safari ndefu kuelekea Spartak Moscow lakini macho ya wengi yataangazia michuano yao miwili dhidi ya washindi wa Ligi ya mabingwa wa mwaka 2011.
Kibarua cha Manchester City kimefanywa kua kikali sana kwa sababu ya vipimo vya UEFA kulingana na jinsi klabu hio ilivyoweza kushiriki mashindano ya Ulaya msimu uliopita na kuonekana kuwa kiwango chake ni cha chini, kwa hiyo Man.City inakabiliwa na kazi kubwa.
Msimu uliopita ilipopangwa na klabu iliyomaliza kwenye fainali Bayern Munich, Napoli ya Italia na Villarreal ya Uhispania mabingwa wa England walishindwa hata kufikia hatua ya kuondoana ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano haya.
Arsenal imepangwa katika timu nane bora kutokana na kile UEFA ilitaja kama muendelezo wa kufanya vizuri katika mashindano yaliyopita.
Mabingwa watetezi Chelsea, Barcelona, Real Madrid, Manchester United, Porto na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vikuu na hivyo vimewekwa katika droo kwa hadhi yao ya kua vilabu bora barani Ulaya.
Kati ya vilabu 32 vilivyopangwa katika droo hii 12 vimewahi kushinda na timu tatu ndipo zimeingia kwa mara ya kwanza.
SOURCE:http://www.bbc.co.uk/swahili
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed