MAYWEATHER AKIFURAHI BAADA YA KUTOKA GEREZANI
Bondia maarufu wa marekani Floyd mayweather ametoka akiwa huru katika gereza la Las vegas leo asubuhi kwa saa za marekani baada ya kutumikia kifungo cha miezi miwili kwa kosa la kumpiga mpenzi wake wa zamani mbele ya watoto wao.
Bondia huyo bingwa ambaye hajawahi kupoteza pambano lolote alipokelewa kwa shangwe na familia zipatazo ishirini pamoja na marafiki akiwemo rapa maarufu wa nchini marekani 50 cent wakati anatoka katika gereza la Clark County Detention Centre
Floyd mayweather mwenye umri wa miaka 35 sasa aliingia katika gari lake ndogo la kifahari aina ya Bentley na kujiendesha mwenyewe kuelekea nyumbani kwake.Alitumikia kifungo chake cha miezi miwili kati ya mitatu aliyohukumiwa kwa kosa la kumshambulia mchumba wake Josie Harris uku watoto wao watatu wakiwa wanaangalia.
Yupo huru kwa sasa na anaruhusiwa kuendelea na shughuli zake za ngumi kama kawaida alisema mwanasheria wake na kuendelea kusisitiza kwamba maisha ya jela hayakuwa mazuri kwa bondia huyo kwa sababu chakula na maji ya gerezani hayakukidhi mahitaji yake ya mfumo wa chakula anachopaswa kula bondia huyo, pia hakupata sehemu nzuri ya kuweza kufanyia mazoezi hivyo kuweza kuhatarisha afya yake.
Mambo mengi yametokea wakati bondia huyo akiwa gerezani tangu alipofungwa tarehe 1 june,2012 , akiwa katika chumba cha gereza ambacho hakina Runinga ameshindwa kuona pambano la mpinzani wake mkubwa manny pacquiao alipopoteza pambano lake la WBO kwa kupigwa kwa utatanishi na bondia wa marekani Timothy Bradley
Mayweather ambaye pia anafahamika kwa jina la utani ''Money'' hakuwepo kusherehekea mwezi uliopita wakati gazeti la Forbes lilipomtangaza yeye kuwa mwanamichezo aliyelipwa zaidi kwa mwaka 2011 pia alikosa kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa mpenzi wake Shantel Jackson pamoja na marafiki zao.
Mapromota wa bondia maarufu wa ufilipino manny pacquiao wanapanga kuandaa pambano litakalopigwa tarehe 10 mwezi novemba katika ukumbi wa MGM Grand Garden ulioko Las vegas Nevada
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed