Thursday, August 02, 2012

KUTOKA AZAM FC


Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na kocha Stewart John Hall kutoka nchini uingerezaulisitishwa rasmi jana Tarehe 31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall, na inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika mudawote aliofanya kazi kama kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.

Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu,Mashindano ya Urafiki na Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha wotewaliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.

Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na inatarajia kuwa ipo siku katika siku za usoni kocha Stewartatarudi tena kufanya kazi na Azam FC.

Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri nikuwa, mrithi wa Stewart Hall atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na Stewart Hallkwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC)

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala

Imetolewa na Utawala

Azam FC


Ufafanuzi juu ya suala la mchezaji Mrisho Halfani Ngasa
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekanakupotoshwa
1. Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa sabamchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopokwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwailikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi yamwenzake.

Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa hakikwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.

Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidiekushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyoteambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FCyazingatiwe.

2. Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishina kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbewao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yangahaikuwa tayari kuboresha ofa yake.

3. Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekitiwake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yangahawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.

4. Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana nakutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopokwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)

5. Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja nastahiki zake nyingine zote za kimkataba

6. Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwaNgasa kama angebaki.
7. Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. KamaNgasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FCitawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC

8. Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatunasababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni nakutumikia adhabu.

9. Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda woteuliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wanidhamu.

10. Kwa kuwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzikama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
a. Kupelekwa kwa mkopo Moro United?
b. Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
c. Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabuyake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juusana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung’ata maneno. AzamFC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendeleekuwa na moyo huo.

Imetolewa na utawala.
Azam FC

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed