Bocco arejea Azam FC. Azam FC yakataa kumtoa kwa mkopo SUFC

Mchezaji John Bocco amerejea kwenye kikosi cha Azam FC baada ya majaribio ya wiki mbili ambayo yaliishia kwakukubalika na kocha mkuu wa Super Sport United FC Gavin Hunt lakini bahati mbaya uongozi wa SUFC ulishindwakutoa ofa ya kueleweka kwa John Bocco na Azam FC
SuperSport United FC ilimtaka Bocco kwa mkopo huku wakisema kuwa kwa sasa hana uwezo wa kuanza kwenyekikosi cha kwanza cha timu yao. Lakini pia SUFC ilishindwa kuweka wazi maslahi ya mchezaji. Maelezo ya Uongoziwa SuperSport United FC ilikuwa ni kumuomba Bocco kwa mkopo kwa kuwa wanahitaji kumuona kwanza akifungakwenye ligi ya Afrika ya Kusini kabla hawajafikiria ofa ya kumnunua.
Wakala wa mchezaji John Bocco Bw. Yusuf Bakhresa aliwataka Supersport United kumuonesha mkataba ambaowataingia na John Bocco na kueleza maslahi ambayo watakuwa wakimlipa lakini ilishindikana zaidi ya kusisitizakuwa wanahitaji muda kabla hawajaingia mkataba mzuri na Bocco.
Yusuf hakufurahishwa na kitendo hicho na aliwataka SUFC kuwa wawazi kama wanamtaka John Bocco na watoe ofaitakayoizidi Azam FC vinginevyo itakuwa vigumu kumpata.
Azam FC imeamua kubaki na nyota wake huyu mwenye umri wa miaka 23 lakini milango ipo wazi kwa SuperSportkuendelea kumfuatilia na itakapotokea kuwa wamejiridhisha na kiwango chake basi walete ofa yao.
John Bocco binafsi baada ya kurejea nchini alisema amefurahishwa na mazingira ya Supersport United lakiniakaomba kuwa angependa kupata maslahi makubwa zaidi ya Azam FC vinginevyo haoni sababu ya kwenda Afrika ya Kusini bila maslahi mazuri kwani Azam FC sasa ni timu kubwa Afrika Mashariki na mwakani itashirikimashindano ya shirikisho barani Afrika.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed