MOUSA DEMBELE
Klabu ya Tottenham imepata idhini ya kuendelea mbele na mipango yake ya kushauriana na kiungo cha kati wa klabu ya Fulham, Moussa Dembele, kufuatia vilabu hivyo kuafikiana juu ya malipo ya kumnunua mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa Ubelgiji yumo katika hali ya kuhudumu mwaka wake wa mwisho katika mkataba na timu hiyo ya Fulham inayochezea uwanja wa Craven Cottage, na hakushiriki katika mechi ya kombe la Capital One dhidi ya Sheffield Wednesday, wakati timu yake iliposhindwa.
Meneja wa Fulham, Martin Jol, amesema Dembele, mwenye umri wa miaka 25, yumo katika hali ya kupimwa hali yake ya afya katika klabu ya Tottenham.
Dembele aliingia Fulham kutoka klabu ya Uholanzi ya AZ Alkmaar, kwa gharama ya pauni milioni 5, mwaka 2010.
Hayo yakiendelea, Fulham imekuwa katika hali ya kushauriana na Kieran Richardson, baada ya kuelewana na Sunderland kuhusu kitita kinachohitajika kumpata mlinzi huyo.
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill alithibitisha kwamba tayari wamekubaliana juu ya kiwango cha pesa ambazo Fulham watatoa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed