SERENA
Katika mashindano ya Olimpiki Serena Williams amejizolea medali ya dhahabu kwa kumshinda Maria Sharapova 6-0, 6-1.
Mchuano huo ulionekana kuegemea upande mmoja ambapo Sharapova hakuonyesha kiwango kilichoonyeshwa na Serena katika fainali ya Tennis ya wanawake katika mashindano ya Olimpiki.
Serena Williams ameondoa rekodi ya Suzanne Lenglen ya 6-3, 6-0 dhidi ya Dorothy
Holman kwenye mashindano kama haya ya mwaka 1920 mjini Antwerp.
Ushindi wa mwanamke huyu kutoka Marekani uliotokea mwezi mmoja tangu ashinde taji la Wimbledon ambako alishinda kwa mara ya tano pia unamfanya kua mwanamke wa pili kushinda mashindano makubwa kiwango cha Grand slam pamoja na dhahabu kwenye Olimpiki.
Serena mwenye umri wa miaka 30 anafuata mfano wa Bingwa wa zamani kutoka Ujeremani Steffi Graf, aliyepata ushindi kama huu mnamo mwaka 1988 aliposhinda mataji matano mwaka huo mmoja.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed