Timu ya mpira wa kikapu ya Marekani maarufu kama Dream Team leo imefanikiwa kusogelea katika fainali ya mashindano ya olympic kwa upande wa mchezo huo baada ya kuichapa bila huruma timu ya mpira wa kikapu ya Argentina kwa vikapu 126-97
Haikuwa kazi rahisi kwa marekani kuweza kupata ushindi huo kwani Argentina walikuwa makini na walionyesha kila sababu ya kutaka kushinda pambano hilo na mpaka wanakwenda mapumziko marekani ilikuwa inaongoza kwa vikapu 60-59.
Ilipoanza robo ya pili marekani iliwashambulia argentina na kuweza kushinda pointi 42-17, wakati Kevin Durant akifunga pointi 3 mara tano kutoka katika umbali mrefu kitu ambacho kiliwafanya wa Argentina waanze kucheza rafu muda mwingi wa mchezo huo.
Hali hiyo ilibadilika katika robo ya tatu wakati LeBron James alipofunga pointi saba za haraka haraka zikiwemo pointi tatu zilizowafanya wawe mbele kwa pointi 67-62 kabla ya Durant kufunga tena kwa umbali mrefu na kufanya marekani kuwa mbele kwa pointi 85-68.
Mpaka pambano hilo linamalizika marekani walikuwa wanaongoza kwa kufunga vikapu 126-97. Wachezaji walioongoza kwa kufunga pointi nyingi ni Durant aliyefunga pointi 28, James18 na Chris Paul 17. Manu Ginobili aliiongoza Argentina kwa kufunga pointi16 na Carlos Delfino alifunga13.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed