
VICTOR MOSES
Timu ya Chelsea imetangaza kukamilisha usajili wa mchezaji Victor moses kutoka katika klabu ya Wigan Athletic kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi.
Moses mwenye umri wa miaka 21 amekamilisha usajili wa chelsea akiungana na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa katika klabu hiyo wakiwemo Cesar Azpilicueta, Marko Marin na Edin Hazard ambao wote walitua katika klabu hiyo
Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Crystal palace ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Nigeria alijiunga na Wigan mwaka 2010 na hakuonyesha makali yake mpaka msimu wa 2010-2011 ambapo alionyesha kiwango cha hali ya juu.
Akiweza kucheza kutoka katika kila upande kama kiungo mshambuliaji na wakati mwingine kama mshambuliaji wa kati ataweza kukisaidia kikosi cha kocha Roberto Di Matteo
Kukamilika kwa usajili huu kumefuatia mchakato wa usajili wa majira ya joto ambapo chelsea walikuwa na mawasiliano na klabu ya Wigan kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed