Kiungo cha kati wa timu ya Chelsea, Michael Essien, amejiunga na timu ya Real Madrid ya Uhispania, kwa makubaliano kwamba ataichezea msimu mzima.
Essien, mwenye umri wa miaka 29, msimu uliopita aliichezea timu yake ya Chelsea mechi 10 tu, baada ya kujeruhiwa misuli mwezi Julai mwaka jana.
Huko Real Madrid atakutana tena na meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho, katika uwanja wa Bernabeu, na ambaye hasa ndiye aliyemsajili katika timu ya Chelsea kutoka Lyon ya Ufaransa mwaka 2005.
Mkataba wa Essien katika uwanja wa Stamford Bridge utakwisha mwaka 2015.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Ghana aliisaidia timu ya Chelsea kupata mataji mawili ya ligi kuu ya Premier na vile vile ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya, na pia ushindi wa Kombe la FA mara nne.
Kiungo cha kati mwenzake katika timu hiyo, Gael Kakuta, mwenye umri wa miaka 21, naye amesajiliwa pia kwa mkopo na klabu ya Uholanzi Vitesse Arnhem, na ataichezea kwa kipindi cha msimu mzima.
Juhudi za Liverpool kumsajili mshambulizi wa Chelsea striker Daniel Sturridge kwa mkopo wa mwaka mmoja, hazikufanikiwa.
SOURCE:http://www.bbc.co.uk/swahili
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed