
Shirikisho la mchezo wa soka nchini Uingereza FA limetangaza kuwa halitamfungulia mashtaka yoyote refa Mark Clattenburg, ambaye anatuhumiwa kutumia lugha ya ubagusi dhidi ya mchezaji wa Chelsea, wakati wa mchuano wa mechi ya ligi kuu ya premier ya England.
Mcheza kiungo wa Chelsea, Ramires, alidai kuwa alisikia refa huyo akimueleza mchezaji mwingine wa Chelsea John Obi Mikel, Nyamasa nyani huyo wakati wa mechi yao tarehe 28 mwezi uliopita dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge.
Lakini shirikisho hilo limesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha ili kumfungulia mashtakab refa huyo.
SOURCE:http://www.bbc.co.uk/swahili
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed