
Kikosi cha timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, U-20 cha Young Africans leo kimetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Stars Rangers ya Kimara katika mchezo wa makundi wa mashindano ya El Talento Soccer Tournament Cup, mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Etihad Stadium - Mwananyamala B.
Vijana wa U-20 wa Young Africans wanashiriki mashindano hayo ambayo mshindi ataibuka na zawadi ya tshs Milioni 3, leo walikuwa wanacheza mchezo wa pili, kufuatia kushinda 2-1 mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu ya Mbagala Market.
Stars Rangers walionekana kukakamia mchezo huo, ukizingatia timu ya U-20 Yanga tangu mwezi wa saba (julai) imeshacheza jumla ya michezo 23, ikishinda michezo 18, sare 4 na kufungwa mchezo mmoja tu dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa utangulizi wa ligi kuu ya Vodacom.
U-20 Yanga waliuanza chezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema, lakini katika dakika ya 23,kiungo Omary Nasry alijikuta akijifunga na kuawapatia Star Ranger bao la kwanza, baada ya kmrudishia mlinda mlango mpira aliopishana nao, hali iliyopelekea Star Ranger kucheza kwa kupoteza muda.
Mlinda mlango wa Stars Rangers alitolewa nje kufuatia kuumia vibaya, baada ya kugongana na mlinzi Zuberi Amir hali iliyopelekea mlinda mlango huyo kupoteza fahamu kwa dakika kadhaa, mpaka alipopatiwa msaada wa huduma ya kwanza na kuzinduka na kupumzika nje.
Mpira ulikwenda mapumziko, U-20 Yanga 0 - 1 Star Rangers.
Kipindi cha pili kilianza kwa kocha mkuu wa U-20 Young Africans kufanya mabadiliko, ya kuwaingiza George Banda, Abdallah Mnguli na Hussein Moishi kuchukua nafasi za Kassim Jongo, Omary Nasry na Said Mashaka.
Mabdiliko hayo yalileta uhai kwa kikosi cha U-20 kwani wachezaji wa Star Rangers wakisaidia na mwamuzi waliamua kupoteza muda kwa kujiadondosha kila dakika huku wakiwa na imani kuwa wameshashinda.
Dakika ya 85, George Banda aliipatia U-20 Yanga bao la kusawazisha kufuatia mpira uliopigwa na Notikely Masasi kuokolewa na walinzi wa Star Rangers kabla ya kumkuta Banda na kuukwamisha mpira wavuni bila ajizi.
U-20 Yanga wangeweza kuondoka na ushindi wa katika mchezo lakini umakini wa washambuliaji katika umaliziaji uliwafanya kukosa mabao mengi ya wazi na mipira zaidi ya mitatu kugonga milingoti na kuokolewa.
Mpaka dakika 90 zinamalizika, U-20 Young Africans 1 - 1 Star Rangers.
Kwa matokeo hayo U-20 Young Africans inaongoza kundi lake kwa pointi 4 na mabao 3 ya kufunga na 2 ya kufunga, ikifuatiwa na Star Rangers yenye point 4, mabao 2 ya kufunga na bao 1 la kufungwa.
Timu mbili za juu kwenye kila kundi zitafuzu hatua ya robo fainali katika mashindao hayo yanayozikutanisha jumla ya timu 16 zilizogawanywa kwenye makundi 4.
U-20 Yanga imebakisha mchezo mmoja wa kumalizia katika kundi lake ambapo itacheza tena siku ya alhamis.
Mchezo wa leo ulihudhuriwa na kocha mkuu Ernie Brands aliyekuwa akitazama vipaji vya vijana.
U-20 Yanga: 1.Yusuph Abdallah, 2.Zuberi Amiri, 3.Said Mashaka/Hussein Moshi, 4.Benson Michael, 5.Issa Ngao, 6.Omary Nasry/Abdallah Mnguli, 7.Rehani Kibingu, 8.Clever Charles, 9.Notikely Masasi, 10.Kassim Jongo/George Banda, 11.Mwinyi Bakari
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed