


LIONEL MESSI AKIWA KATIKA HARAKATI ZAKE KATIKA PAMBANO LA JANA DHIDI YA BILBAO AMBAPO ALIFANIKIWA KUTUPIA KAMBANI BAO 2
Lionel Messi alifunga bao mbili wakati barcelona ikianza vizuri katika historia ya mashindano ya Laliga kwa ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Timu ngumu ya Athletic Bilbao.
Vinara hao wa La liga wameshinda mara 13 na kutoka sare mara 1 katika mapambano 14 waliyocheza na kuwapiku wapinzani real madrid walioshinda mara 12 na kutoka sare mara 2 katika kampeni ya 1991-92.
Lionel messi aliyefunga mara mbili katika mechi 11 za msimu huu amebakiwa na goli 1ili aweze kuifikia rekodi ya Gerd muller ya kufunga magoli 85 kwa klabu yake na timu ya taifa kwa mwaka mmoja rekodi hiyo iliwekwa mwaka 1972.
Barcelona iliongoza kwa magoli 3-0 katika kipindi cha kwanza shukrani ziende kwa magoli ya Gerald pique, messi na adriano.
Kwingineko katika Laliga Valencia wamemtimua kocha wao Mauricio Pellegrino baada ya kukubali kipigo cha nyumbani cha bao 5-2 kutoka kwa Real sociedad ikiicha timu hiyo ikiwa nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed