

Bilionea na mmiliki wa klabu ya Arsenal Alisher Usmanov, amesisitiza kwamba Thiery henry lazima arudi katika klabu ya arsenal na safari hii si kama mchezaji bali kama mmoja kati ya jopo la makocha wa timu hiyo.
Taarifa hiyo imekuwa siku chache baada ya arsenal kutolewa kwa aibu na klabu ndogo ya daraja la pili ya bradford katika mashindano ya Capital one maarufu hapo zamani kama "Carling Cup".
Kocha wa sasa arsenal wenger ana mkataba na klabu hiyo mpaka mwaka 2014 na anaonekana kutokuwa na wasiwasi na kibarua chake kutokana na kukubalika na wawekezaji wengi na bodi ya klabu hiyo na kumekuwa na mashaka juu ya uhusiano wa sasa kati ya kocha mkuu arsene wenger na msaidizi wake Steve Bould katika utendaji wao wa kazi.
Alisher Usmanov ambaye anamiliki asilimia 29 za hisa za klabu hiyo na akiwa pia anapigania kupata hisa nyingi zaidi ameona kuna kocha wa sasa Arsene wenger anahitaji msaada katika safu ya wasaidizi wake.
Usmanov raia wa Russia mwenye umri wa miaka 59 amesema mfaransa Thiery henry ana majukumu makubwa sana ya kufanya katika klabu ya arsenal zaidi ya kucheza mpira wakati atakoporejea kwa mkopo ifikapo mwezi januari kutoka katika klabu ya New York Red Bulls ya Marekani.
Sina mamlaka makubwa sana katika maamuzi ya klabu hii lakini kuna wachezaji wachache ambao nimekuwa nikiwasiliano nao na chaguo langu ni Thiery henry na anatakiwa kujumuishwa katika klabu hii katika jopo la makocha.
Mwangalie Patrick Viera pale manchester city ni Alama ya Arsenal lakini anaisaidia timu nyingine.alisema usmanov.
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed