Monday, January 07, 2013

Azam FC yakaribia nusu fainali Mapinduzi Cup



Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wamejiweka katika nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali yamashindano hayo baada ya kuifunga Miembeni FC 3-1 katika mchezo uliochezwa leo usiku kwenye Uwanja waAmaan, Zanzibar.

Brian Umony pichani juu akiruka mkwanja wa Adeyum Saleh, Picha kwa hisani ya Blogu ya Binzubeiry

Azam FC imepata ushindi huo muhimu na kuongoza kundi hilo ‘B’ kwa kuwa na pointi nne, ikifuatiwa na Miembeniyenye pointi 3, Coastal Union ina pointi mbili huku Mtibwa wakiwa wa mwisho kwa kuwa na pointi 1.

Katika mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa ulianza kwa kasi na dakika ya pili Azam FC walipata bao la kwanzalililofungwa na beki aliyesajiliwa hivi karibuni Jockins Atudo aliyefunga kwa kichwa akimalizia mpira wa konailiyochongwa vyema na kiungo Humphrey Mieno wote kutoka Kenya.

Miembeni walisawazisha goli hilo dakika mbili baadaye, kupitia kwa mchezaji Adeyum Ahmed aliyepiga mpira wakona ambao mwamuzi aliona ulioenda moja kwa moja wavuni.

Kupatikana kwa goli hilo kuliurudisha mchezo huo kuwa wa kasi na kushambuliana zaidi huku wachezaji wa AzamFC, Mieno, David Mwantika, Brian Umony na Khamis Mcha walicheza vizuri kwa kuonana na kutengeneza nafasinyingi.

Safu ya ulinzi ilisimamiwa vizuri na nahodha Himidi Mao, Atudo, Samih Haji Nuhu na Mwantika, tangu muda huowaliweza kuzui mashambulizi ya Miembeni na kuwapa nafasi washambuliaji wa Azam FC kupanda juu nakutengeneza nafasi.

Mshambulia mrefu na mwenye nguvu Gaudence Mwaikimba aliipatia Azam FC goli la pili baada ya kuunganishampira uliopigwa na Mieno na kuwapita mabeki wa Miembieni na kupiga shuti lililotinga moja kwa moja wavuni, golihilo lilizipeleka timu hizo mapumziko Azam FC wakiwa mbele kwa 2-1.

Kipindi cha pili kilianza na sura mpya, timu zote ziliwakosa walimu wake Stewart Hall wa Azam FC na Salum Bausiwa Miembeni baada ya kutolewa na mwamuzi wa mchezo huo Ally Kisaka baada ya kumzonga mwamuzi huyo wakatiwa mapumziko.

Azam FC ilifanya mabadiliko kuimarisha kikosi chake walitoka Mcha dk 60 nafasi yake ikachukuliwa na UhuruSelemani, dk 65 aliingia Seif Abdalah kuchukua nafasi ya Umony, dk ya 82 walitoka Salum Abubakar ‘Sure Boy’ naMieno nafasi zao zikachukuliwa na Jabir Aziz na Ibrahim Mwaipopo.

Mabadiliko hayo yaliongeza nguvu kwa Azam FC na kuinyanyasa ngome ya Miembeni, dk 87 Uhuru aliipatia Azam FCgoli la tatu kwa shuti baada ya beki wa Miembeni kuokoa shuti la Mwaikimba, mpira ukarudi uwanjani ndipo Uhurualitumia nafasi hiyo kuwainua mashabiki wa Azam FC na kumaliza mchezo Azam FC ikipata ushindi huo wa 3-1.

Kwa matokeo hayo Azam FC imejiweka katika nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali ya mashindano hayo ambayomustakabali wake utaamliwa kwenye mechi za Jumatatu ambazo Azam FC itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar hukuCoastal Union wakimenyana na Miembeni mshindi katika mechi hizo ataingia nusu fainali.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amesema matokeo hayo mazuri kwa timu wamebakisha kibarua chakuitoa Mtibwa Sugar ili wavuke na kuingia nusu fainali.

Alisema wataingia katika maandalizi kesho kwa kuwa wanaijua timu hiyo hivyo haitawasumbua sana kuliko kukutanana timu ambazo hawajawahi kucheza nazo.

Azam FC, Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Haji Nuhu, David Mwantika, Jockins Atudo, Michael Bolou, BrianUmony/Seif Abdalah 60’, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ /Jabir Aziz 82’, Gaudence Mwaikimba, Humphrey Mieno/ IbrahimMwaipopo 82’ na Khamis Mcha/Uhuru Seleman 65.

Miembeni, Seleman Hamad, Mfaume Odela, Adeyum Saleh, Salum Haji, Salum Juma, Sabri Ally, Laurent Mugiya,Seleman Haji, Monja Liseki/ Mohamed Salum, Rashid Roshua/Peter Ilunda na Issa Othman.

No comments:

Post a Comment

only comments that are benefial for this blog is allowed