
Timu ya Azam FC imewasili salama visiwani Zanzibar leo tayari kwa kutetea Kombe la Mapinduzi 2013, keshowatacheza dhidi ya Coast Union kwenye Uwanja wa Amaan.
Azam FC ambao ni bingwa mtetezi wa kombe wamewasili mchana na boti ya Kilimanjaro III wakiwa na kikosi kamilichenye waachezaji wote, wazamani na wapya waliosajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili mwezi uliopita.
Timu hiyo ipo kundi B pamoja na timu za Coastal Union, Mtibwa Sugar na Miembeni FC, huku Kundi A linaundwa naSimba SC, Bandari FC, Jamhuri FC na Tusker FC ya Kenya.
Azam FC itakutana na Coastal Unio katika mchezo wake wa kwanza utakaochezwa kesho usiku, mechi ya pili itaikutanisha na Miembeni na mechi ya mwisho ya kumalizia hatua ya makundi itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar katikaUwanja huo.
Mashindano maalumu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar, fainali zitachezwa siku ya MapinduziJanuari 12 usiku, ambapo bingwa atakabidhiwa kombe na kiasi cha fedha.
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Azam FC kushiriki katika kombe hilo linalokutanisha timu za kutoka Tanzania bara na visiwani , ilicheza kwa mara ya kwanza mwaka 2011 ikitolewa katika hatua ya makundi, mwaka 2012 ikatwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Jamhuri ya Pemba kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Amaan.
source:http://www.azamfc.co.tz
No comments:
Post a Comment
only comments that are benefial for this blog is allowed